Videos

Ndugai: Zuio mikutano ya hadhara linahitaji mwafaka


Spika wa Bunge, Job Ndugai

Na Suleiman Msuya

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amesema ingawa msuguano baina ya Serikali na wapinzani kuhusu mikutano ya hadhara na maandamano hauna tija, kuna haja ya kufanya mazungumzo ili kupata mwafaka kuhusu jambo hilo.

Ndugai alisema hayo jana katika Kipindi cha Funguka kilichorushwa na televisheni ya Azam Two kikiongozwa na mmoja wa waandishi wakongwe nchini, Tido Mhando.

“Mimi nashauri mazungumzo yaendelee kama yapo, waone namna gani tunavyoweza kujenga demokrasia yetu ya Kitanzania, lakini kwa kweli kuendelea na kampeni zisizoisha za maandamano na mikutano ya hadhara ni kuwadanganya wananch kwa kueleza mambo ambayo hayapo, kwa sababu kumbuka hii mikutano ni information (taarifa) za upande mmoja tu, upande wa pili hauna fursa ya kubalansi,” alisema Ndugai.

Mbali na msuguano huo, Ndugai pia alizungumzia mambo kadhaa, ikiwamo sakata la Lugumi, mgogoro wa wabunge wa upinzani na uongozi wa Bunge na Serikali kuhamia Dodoma kama inavyonukuliwa hapo chini:

Swali: Unazungumziaje taarifa za vyama vya siasa kutaka kuandamana kwa kile wanachodai kuwa kuna uminyaji wa demokrasia?

Jibu: Hili jambo lina tatizo la utamaduni tu. Tatizo kwa siasa za Tanzania watu wakimaliza uchaguzi wanataka kufanya mikutano ambapo asilimia kubwa ya mikutano hiyo inatawaliwa na maneno ya kashfa na matusi, hivyo hatuwezi kukubaliana na hali hiyo.

Kinachotakiwa ni sisi tufuate utaratibu wa Jumuia ya Madola ili kuruhusu Serikali ifanye kazi kwani asilimia kubwa ya wanaotaka kufanya siasa wanajukwaa la Bunge, hivyo watumie nafasi hiyo kufikisha ujumbe.

Wapo baadhi ya wabunge wanaotumia lugha chafu ndani ya Bunge kwa kuwatukana mawaziri, hivyo watu hao wakipata uwanja wa kusema nje ya Bunge ndio kasi inaongezeka.

Mikutano hiyo asilimia kubwa kinachosemwa hakina ukweli wowote hali ambayo hata ndani ya Bunge inatokea ila zipo adhabu za kikanuni tofauti na huko nje ambako hakuna kanuni.

Aidha, changamoto iliyopo ni kuwa yanayosemwa huko nje hakuna mtu wa kujibu, hivyo jamii inaaminishwa jambo ambalo linawezekana kuwa na majibu. Naamini mazungumzo bado yanahitajika ili kuhakikisha kuwa muafaka unafikiwa kwani hakuna sababu ya kuendeleza malumbano ambayo hayana tija.

Swali: Ipo hoja ya Lugumi ambayo imeonekana kuzimwa katika mazingira ya kutatanisha hasa baada ya wabunge wa upinzani kutoka nje ya Bunge. Wewe unazungumziaje uamuzi huo?

Jibu: Ninavyojua sakata la Lugumi halijapita bado baada ya kamati ndogo kufanya kazi kwa kupita nchi nzima na kuona kuwa vifaa vilipelekwa na havijafanya kazi hivyo Naibu Spika aliagiza baadhi ya mapungufu kutatuliwa. Wabunge wa upinzani ambao walitoka wametolewa kwa makosa ambayo walifanya ila hawa wengine walikuwa wanatoka katika mgomo wao.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), itapata nafasi ya kutoa taarifa yake, lakini taarifa rasmi kuhusu Lugumi itawasilishwa bunge lijalo na wapinzani wakiwapo na watapata fursa ya kuchangia kinagaubaga.

Swali: Je, unafikiria utachukua mkondo gani ili kumaliza hali hii ya kutoelewana baina ya wapinzani na uongozi wa Bunge.

Jibu: Kusema kweli katika mambo ambayo yananinyima usingizi ni hali hii ya kutofautiana baina yetu na wabunge, hivyo nafikiria kuwepo na watu wazoefu na wastaafu kama spika mstaafu Anne Makinda na wenzake waweze kutusaidia kutatua changamoto zilizopo.

Aidha, kuna dhana kuwa Naibu Spika Dk Tulia Ackson ujio wake umekuwa na maswali mengi na hofu kwa baadhi ya wabunge kuamini kuwa atakuwa anatetea maslahi ya upande ambao umemteua. Ni kweli kuwa hali hiyo haijawahi kutokea hata mabunge ya Jumuia ya Madola yamekuwa yakitumia mfumo wa kuhakikisha kuwa Naibu Spika anakuwa ni mbunge wa kuchaguliwa na si kwa mfumo wa Dk Tulia.

Sisi hatupokei maagizo kutoka popote pawe Ikulu au kwa Rais moja kwa moja ila tunafanya kazi kwa kufuata kanuni za Bunge ambazo zinatumika kila siku. Napenda wabunge watumie nafasi zao kuibana Serikali kupitia Bunge na wakisema tunafanya kwa msukumo wa Serikali tunapaswa kuuliza ni mbunge yupi ameuliza swali tukakataa kuwapa nafasi ya majibu.

Swali: Kitendo cha Bunge kutooneshwa moja kwa moja unakizungumziaje?

Jibu: Kwa sasa ndio uamuzi ambao umefikiwa, hivyo tunaendelea na utaratibu huo kwani tumeona faida yake tofauti na zamani ilivyokuwa ambapo wabunge walikuwa wanatumia vibaya nafasi hiyo. Wabunge wakijua wanaoneshwa moja kwa moja wanatumia nafasi hiyo kuleta usanii na kuwa ni tatizo kubwa lakini tukiwa kama kamati utulivu unakuwepo.

Swali: Baada ya Serikali kutangaza kuhamia Dodoma, Bunge nalo limeanza kupeleka vikao vyao huku kwa nini imekuwa hivyo?

Jibu: Sisi Bunge tumekuwaDodoma kwa muda mrefu ila changamoto ilikuwa ni kufanya vikao vya kamati Dodoma kwani kamati zilikuwa za watu wachache hivyo kuhamishia watendaji Dodoma wakati wa kamati ilikuwa ngumu. Kwa sasa tumeamua kuanzia sasa kila kitu ni Dodoma na asilimia 99 ya watumishi wa Bunge watakuwa Dodoma kiofisi na makazi. Naamini watabakia asilimia moja tu ambayo itakuwa inashughulikia mambo machache kama wabunge wakitaka kusafiri, wakiumwa na baadhi ya mambo ambayo yatahitaji kutatuliwa Dar es Salaam. Kwa mimi ambaye ninatoka Dodoma naunga mkono uamuzi wa Rais John Magufuli, kuhamishia shughuli za Serikali Dodoma kwani ni jambo jema.

Swali: Bunge lako limekuwa na utoro wa hali ya juu wewe umejipangaje kutatua au kuondoa hali hiyo?

Jibu: Hili la utoro ni kweli lipo ila si kwa Tanzania pekee, nchi nyingi hali hiyo ipo mfano nilikuwepo Kenya wakati fulani na kushuhudia uwapo wa wabunge 14 tu bungeni.

Wapo wabunge ambao wanaingia na kusaini halafu wanaingia katika mgahawa na baabaye wanaondoka. Pia lipo tatizo la wabunge wafanyabiashara, hawa nao hawatulii bungeni. Muda mwingi wanashughulika na biashara zao na jambo hilo linakatisha tamaa kwani hawataekeleze majukumu yao ipasavyo.

Swali: Wabunge wamekuwa wakisema kuwa posho zinazotolewa ni nyingi na wengine wamediriki kusema hawatachukua hili unalizungumziaje?
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment