Videos

Mmiliki wa shule ajilipua kwa petroli



Joyce Anael, Moshi

MFANYABIASHARA na mmiliki wa Sekondari ya Merinyo wilayani hapa, Roman Shirima (74) amejiua kwa kujimwagia petroli na kujiwasha moto kwa kiberiti.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema mfanyabiashara huyo alijiua juzi saa 11:25 alfajiri nyumbani kwake Mjohoroni, kata ya Msaranga Ng’ambo, mjini hapa.

Kamanda Mutafungwa alisema mfanyabiashara huyo aliungua kwa kiwango kikubwa na kusababisha kifo chake na kuhusu chanzo cha tukio hilo, alisema hakijafahamika na Polisi inaendelea na uchunguzi.
 
Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya wananchi mkoani Kilimanjaro, walieleza kusikitishwa na kifo hicho huku wengine wakidai kuwa siku moja kabla walikutana naye na aliwaeleza mipango yake ya kuboresha shule yake.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Kilimanjaro ya Mawenzi, kusubiri taratibu za mazishi.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment