Videos

Teknohama yakomaza ulimwengu wa upweke



William Shao

WATAFITI wamegundua kuwa ijapokuwa kuna njia na vifaa vingi vya mawasiliano kuliko wakati mwingine wowote katika historia, hakuna kipindi amba­cho wanadamu ni wapweke kama ilivyo leo.

Simu za mkononi, ujumbe mfu­pi (SMS), Whatsapp, Instagram, baruapepe, Facebook, Telegram, vituo vya mawasiliano na vituo vya maongezi—hakujawahi kuwa na kipindi chochote katika histo­ria ya mwanadamu ambapo kuna njia nyingi za kuwasiliana kama ilivyo sasa.

Pamoja na njia zote hizo, watafi­ti wanadai kuwa katika dunia hii yenye njia nyingi za mawasiliano, watu wengi, vijana kwa wazee, ni wapweke mno.

Watafiti wawili—John T. Ca­cioppo na William Patrick—ka­tika kitabu chao, ‘Loneliness— Human Nature and the Need for Social Connection’, wamezun­gumza kwa undani kuhusu up­weke huo.

Wamezungumzia uchun­guzi mmoja uliosema kwamba “kutumia sana Intaneti badala ya kuzungumza na mtu moja kwa moja, kunaweza kufanya watu wajitenge na jamii na pia kuongeza hali ya kuhuzunika.”

Hekaheka za maisha ya kisasa zinafanya iwe vigumu kwa watu kuwasiliana kwa njia inayofaa. Kwa kawaida, unadai utafiti huo, huwezi kuona uso unaotabasamu na upendo unapowasiliana na mtu kupitia simu au kwa kutuma ujumbe kupitia kompyuta.

Mambo yaliyotajwa hapa juu hutokea pia katika familia. Ka­tika nyumba nyingi, watu wa fa­milia huja na kuondoka bila kula pamoja au kuzungumza pamoja. Vijana wana kompyuta na simu zao wenyewe nao hujitenga na watu wengine wa familia. “Licha ya kwamba wana vifaa vingi vya mawasiliano, vijana wengi huji­hisi wakiwa na wapweke,” wa­nasema watafiti hao.

Siku hizi hata ndoa zinaweza kuhatarishwa kwa sababu ya wenzi kujihisi wakiwa, wapweke. Wenzi wa ndoa wasipowasiliana, wanaweza kuwa katika nyumba moja lakini kila mtu anaishi mai­sha yake. Kuhisi upweke huku ukiwa unaishi na mwenzi wa ndoa ni upweke unaofadhaisha sana. Mbali na vitu vingine vin­gi, kuwepo kwa vifaa vingi zaidi vya mawasiliano kunaweza ku­katiza mawasiliano kati ya mzazi na watoto na hivyo kufanya hisia za upweke ziongezeke. Pia wase­ja wengi wanatamani kuwa na mwenzi, lakini mahitaji yao ya kihisia hayatoshelezwi.

Upweke umekuwa tatizo kub­wa katika jamii, tatizo ambalo linaweza kusababisha uraibu wa pombe, kula kupita kiasi, ku­tumia dawa za kulevya, kufanya ngono za ovyo, na hata kujiua.

Nchini Japani, Profesa Tetsuro Saito alisema: “Simu za mkononi na vifaa vingine vinapunguza uwezo wetu wa kuwasiliana na wengine kwa hisia.”

“Watoto wanaeleza ni kitu gani muhimu sana kwao, baada ya maisha yao, kinachofuata kwa umuhimu ni simu za mkononi,” akasema Masashi Yasukawa, Mkuu wa Baraza la Taifa la Ushau­ri wa Mitandao nchini Japani, al­ipokaririwa na gazeti ‘The Sydney Morning Herald’ la Australia,la Januari 12, 2008. Utafiti mwing­ine nchini huo ulichapishwa na gazeti ‘The Sunday Telegraph’ uli­gundua hivi: “Teknolojia . . . in­awafanya watu wajitenge kihisia. Watu … hutumiana ujumbe mfupi au barua-pepe badala ya kuzungumza moja kwa moja.”

Utafiti unaojulikana kama ‘Loneliness and Mobile Phones’uliofanywa nchini Uturuki kwa kufanyiwa wanafunzi zaidi ya 500 wa Chuo Kikuu cha Firat, uligundua kuwa kuna uhusi­ano mkubwa kati ya matumizi makubwa ya simu za mkononi na kuhuzunika pamoja na kuwa na soni au haya.

Vinajana hawa kila mmoja akiwa na chombo chake cha mawasiliano ambacho kinaelezwa katika utafiti kusababisha upweke na haya au soni.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment