Videos

Polisi: Lema hakugoma kula, hatumshtaki


Seif Mangwangi, Arusha

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limeamua kuondoa nia yake ya awali ya kumfikisha mahakamani Mbunge wa Arusha mjini, Godbles Lema kufuatia kudaiwa kugoma kula chakula wakati akiwa katika mahabusu ya Polisi jijini hapa.

Akizungumza na JAMBO LEO jijini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema jana wameamua kuondoa nia hiyo baada ya kugundua kuwa Lema alikuwa akila chakula kupitia kwa mahabusu wenzake.

Alisema taarifa ambazo zililifikia jeshi hilo ni kwamba mbunge huyo alikuwa akigoma kula chakula ambacho alikuwa akipelekewa na mke wake na alipokuwa akibembelezwa akile alikikataa hivyo jeshi hilo kujipanga kumfikisha mahakamani.

“Hata hivyo uchunguzi tulioufanya tulikuja kugundua kuwa baada ya yeye kugoma kula chakula cha mke wake na kubembelezwa mara kadhaa na kukataa, lakini alikuwa akila chakula kwa siri kupitia mahabusu wenzake aliokuwa nao ndani,”alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment