Videos

UVCCM wazidi kuvurugana



UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM), umesema utaendelea kuchukua hatua dhidi ya makada wake mbalimbali watakaobainika kuhusika na ufujaji wa mali za umoja huo huku wakitumia nafasi hiyo kuonesha ujumbe mfupi wa simu ya mkononi uliotumwa na James Mwakibinga wa kuomba nafasi ya Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji.

Kwa mujibu wa UVCCM, ni Mwakibinga hakupewa nafasi hiyo aliyoiomba na hivyo ameamua kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutoa taarifa ambazo si sahihi na zenye mlengo wa kuleta chuki na mvurugano ndani ya umoja huo.

Kutokana na hali hiyo, UVCCM kupitia Kaimu Katibu Mkuu wake, Shaka Hamdu Shaka wametoa siku saba kwa Mwakibinga kuthibitisha madai yake yanaoonesha kutaka kuvuruga umoja huo na iwapo atashindwa kuthibitisha watamfikisha mahakamani.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Shaka alisema umoja huo umesikitishwa na taarifa za upotoshaji ambazo zimetolewa na Mwakibinga kuhusu mali za chama hicho na kueleza wazi umoja huo umekuwa ukichukua hatua kwa mujibu wa miongozo ya kanuni dhidi ya wanaobainika kufuja mali zake na kwamba, wataendelea kujitathmini ili kubaini maeneo yote ambayo yana harufu ya ufisadi.

"Kazi ya kuisafisha UVCCM imeanza siku nyingi, ambapo umoja huo ni moja ya jumuiya za chama uliwasilisha kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ombi la kupewa wakaguzi ili kukagua mambo mbalimbali.

"Hivi karibuni nilipokea ujumbe mfupi (SMS), kutoka kwa Mwakibinga akiomba kuteuliwa kuwa Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM, wakati umoja huo ukielekea kwenye kikao cha baraza kuu. Hivyo, baada ya kukosa nafasi hiyo aliamua kuitisha vyombo vya habari leo (jana), na kuanza kutoa taarifa za uongo ambazo hatutazifumbia macho,"alisema.

Shaka alisema Mwakibinga katika ujumbe huo aliambatanisha wasifu wake uliokuwa na mambo mbalimbali, lakini hakumjibu na anashangazwa na hatua alizochukua za kushambulia umoja wa vijana kwa tuhuma za uongo na kujiita kada wa umoja huo akiwa hajulikani na hana sifa.

"SMS yake hii hapa alianza kwa kunisalimia na kuniambia kuwa, ananitakia kila la heri katika kikao cha baraza kuu ambacho kitanithibitisha kuwa katibu mkuu na ananiomba nimchague yeye kuwa katibu wa uhamasishaji, ananihakikishia tutafanya kazi na kisha akatuma wasifu wake.


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment