Videos

Wengi hawajui kupatwa kwa jua


Richard Mwaikenda, Mbarali

WAKAZI wengi wa Rujewa, wilayani Mbarali, waliofika kuangalia eneo ambalo jua litapatwa na mwezi, wamekuwa hawaelewi jinsi tukio hilo litakavyokuwa.

Baadhi ya wakazi hao waliohojiwa na mwandishi wetu katika eneo hilo la Relini, kwamba waeleze ?kitakachokea (kesho), leo walijibu kuwa hawaelewi.

Jumanne Mavunde (45), aliyekutwa akiwa amejiinamia kwenye baiskeli yake, alisema kuwa hata yeye hajui kitakachotukia ila alisikia alipofika pale kuwa eti jua litapatwa na kwamba walioandaa ndiyo wanaojua.

Naye Halima Abbas (35) ambaye ana elimu ya sekondari kidato cha nne, alisema kuwa anasikia tu kwamba kuna kupatwa kwa jua lakini hajui ni kitu gani. Pia alisema hakumbuki kama somo hilo alilisoma akiwa shuleni.

Mkazi wa Rujewa mwenye jamii ya kimasai, Joshua Ole Kaulule, alijibu kuwa  anachojua ni kwamba(kesho) leo, jua na mwezi vitagongana na kusababisha giza zaidi ya hapo haelewi.

Mwanamke mfanyabiashara wa mchele, Heri Kiluswa, alisema kuwa yeye alikuwa anapita barabarani alishawishiwa kwenda pale baada ya kuona watu wengi wamekusanyika, lakini haelewi ni kitu gani kitanyika na alipouliza aliambiwa kuwa kuna tukio la kupatwa na jua, ila bado haelewi ni jambo gani.

Mwanafunzi wa Darasa la saba katika Shule ya Msingi Ihanga, Goodluck Mwanpasha (13), alisema kuwa hajui lolote na hata shule hajawahi fundishwa na baada ya kuona watoto wenzie wanamcheka alitimua mbio na kutokomea.

Lakini Mwananfunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Ibala, Adamu Chengula alikiri somo hilo kufundishwa, hivyo kujibu kiufasaha kwamba kupatwa kwa jua ale inapotokea  Dunia, Mwezi na Jua kuwa kwenye mstari mmoja na mwezi ukiwa katikati huzuia miale ya jua na kusababisha giza katika uso wa dunia.

Mwandishi wetu alipata wasaa wa kuzungumza na Pasvolo Mwinuka Mwalimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Idara ya Sayansi,  ambaye alieleza kitaalamu juu ya kupatwa kwa jua.

Alisema kuwa tukio hilo hutokea dunia, mwezi na jua vinapokuwa kwenye mstari mmojo na mwezi kuwa kati hivyo kuziba mwanga jua kuifikia dunia.

Alija aina tofauti za kupatwa kwa jua kuwa ni. Mosi; Kuziba kabisa mwanga wa jua kunaitwa kupatwa kwa jua kikamilifu (Total Solar Eclipse).

Pili;Kiasi kidogo cha mwanga wa jua kuifikia dunia (Partial Solar Eclipse) na miale ya jua itakuwa imezibwa kwa kiasi kikubwa kwa asilimia 97, kitendo ambacho hutengeneza muonekano wa mfano wa pete na tukio hili ndiyo litakalotokea leo Rujewa. Kupatwa kwa jua kutaanza saa 4 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Alisema kitendo hicho duniani kitatokea hapa nchini eneo la Relini Rujewa, mkoani Mbeya na kutaja  maeneo mengine patapoonesha kwa kiasi tukio hilo ni wilayani Wanging'ombe, Njombe, Karibu na Ziwa Tanganyika pamoja na baadhi ya Nchi ya DRC Congo.

Naye Mjumbe wa Kamati ya Utalii ya Wilaya hiyo, alisema kuwa maandalizi yanaenda vizuri na tayari wametoa elimu kwa wananchi juu ya tukio hilo muhimu na la kihistoria katika wilaya hiyo na njci kwa ujumla.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Jumanne Maghembe ambapo pia atakuwepo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makalla na viongozi wengine.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment