IGP Mangu |
JESHI la Polisi limeanza msako wa kukamata watu wanakwenda kulala nyumba za wageni muda wa kazi.
Msako huo ambao unaoelezwa ni agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alilolitoa kwa wakuu wa wilaya jijini humo ulianza juzi Tegeta, Kinondoni.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa wa JAMBO LEO ambaye alishuhudia tukio la watu kukamatwa katika moja ya nyumba za wageni wakati hayo yakitokea walidhani wanaokamatwa ni wahalifu au majambazi, lakini walivyohoji walielezwa kuwa polisi walivamia nyumba hiyo ya wageni na kusomba watu wote waliokuwa wamelala saa za kazi.
“Juzi nilikuwa Tegeta nikaona gari la Polisi linasomba watu kutoka moja ya nyumba za wageni kwa kuwa walikuwa wengi tukadhani majambazi lakini tulivyouliza, wakasema ni watu wanaolala mchana bila kufanya kazi,’’ alisema mtoa habari huyo.
Alisema baadhi ya watu walijaribu kuhoji baada ya Polisi kuondoka kutokana na kuhofia kuchanganywa katika kundi la watu wasiofanya kazi, ndipo wakaelezwa kuwa ni agizo la Makonda kwamba wanaolala na kufanya ngono muda wa kazi wakamatwe.
DC Kinondoni
JAMBO LEO lilimtafuta Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi ili kupata ufafanuzi kuhusu agizo hilo linalodaiwa kutolewa na wakuu wa wilaya baada ya kupokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alisema: “Watafutwe polisi.”
Hata hivyo, Mkuu huyo wa wilaya hakukubali wala kukanusha kuwepo kwa operesheni hiyo, lakini akasema suala lolote la kukamatwa watu polisi ndio wanaopaswa kulitolea maelezo.
“Sasa huyo aliyekamatwa akiwa amelala hafanyi kazi na aliyekusimulia pia walipaswa watoe majibu ya kina, alipaswa kwanza kuulizwa yeye hilo suala na kama amekamatwa na polisi ufafanuzi unapaswa kufanywa na Jeshi hilo si mimi,’’ alisema.
Kamanda wa Jeshi hilo Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro alikiri kuwepo kwa operesheni hiyo jana asubuhi katika kipindi cha Joto la Asubuhi kinachorushwa na Redio ya Efm.
Siro alisema operesheni hiyo inalenga watu wanaozurura na wasiojituma muda wa kazi.
0 comments:
Post a Comment