WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Sim¬bawene amesema kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuifanya Dodoma kuwa Makao Makuu, mji huo unaelekea kuwa na hadhi ya jiji.
Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje (CCM), Simbachawene alisema mji huo una kilomita za mraba 250,000 ambazo zinatosha kuufanya kuwa jiji.
“Kwa jitihada za kuhamia Dodoma zinazofanywa na Serikali hii ya Awamu ya Tano,lazima Dodoma iwe Mamlaka ya jiji,hata ukiangalia kigezo cha ukubwa,utaona Dodoma ina ‘square ‘ kilomita 250,000, ni nyingi, hivyo Dodoma inafaa kuwa jiji.” alisisitiza Simbachawene
Katika swali lake hilo, Lubeleje alitaka kujua lini Serikali itaitangaza Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuwa Halamshauri ya Jiji.
Awali, akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Selemani Jafo alisema su-ala la kuufanya Mji wa Dodoma kuwa jiji halina mashaka .
“Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu mbalimbali ili Mji wa Dodoma ufikie hadhi ya kuwa jiji hususan katika kipindi ambacho Serikali sasa inahamia Dodoma.” alisema Jafo
Katika swali la msingi, Mbunge wa Moshi Mjini Raphael Michael (Chadema) alitaka kujua lini Serikali itaitangaza Manispaa ya Moshi kuwa Jiji wakati Halamshauri ya Manispaa hiyo ilianza mchakato huo mwaka 2012, baada ya kupata baraka za Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kiliman¬jaro (RCC) na Kamati ya ushauri ya Moshi (DCC).
0 comments:
Post a Comment