Videos

Kituo cha Mabasi Ubungo kugeuzwa jengo la biashara


MEYA wa Halmashauri Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita alisema Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha Ubungo kitapohamishwa eneo hilo litafanyiwa ukarabati na kugeuzwa jengo la biashara (business park) na litachangia fursa za ajira na uchumi kwa nchi.

Akizungumza na gazeti hili, Meya huyo alisema kituo hicho kitapohamia Mbezi Luis wilayani Ubungo mchakato wa ukarabati utaanza ili kufanikisha jengo hilo kufunguafursa hizo kwa kiasi kikubwa ikiwamo kuingizia Jiji mapato ya kutosha.

“Kituo kikihamia Mbezi Luis Jiji litasimamia ujenzi wa jengo kubwa la biashara... likishakamilika vijana watapata ajira na mapato yatakuwa mengi,” alisema. Meya Mwita alisema jengo hilo litakapokamilika litafungua fursa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza biashara mbalimbali.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment