Kwa mujibu wa Sheikh Jalala, picha hiyo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha nguruwe akiwa amekaa juu ya nyumba takatifu ya Makka (Al-kaaba) na kuielezea hali hiyo kwamba ni hatari na udhalilishaji.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Sheihk Jalala alisema ni muhimu TCRA imchukulie hatua stahiki kama walivyochukuliwa hatua watu wengine waliofanya makosa katika masuala ya mitandao.
“TCRA ni wajibu wao kuangalia mambo yaliyokwenda kinyume katika mitandao ya kijamii, wachukue hatua za haraka, kwasababu tumeona matukio madogo tu yaliyotokea mamlaka imechukua hatua za haraka,”alisema.
Alisema udhalilishaji huo ni tukio kubwa na mamlaka hiyo haipaswi kulinyamanzia suala hilo, huku huku akivitaka vyombo vya usalama kutambua kwamba matukio kama hayo yanaweza kuenea na kuvunja heshima ya vitu vinavyoheshimiwa na kusababisha mvutano.
Alisema ni vema mamlaka ikaliangalia hilo kwa jicho la pekee ili tukio hilo lisihatarishe maisha. “Al-Kaaba ni nyumba takatifu sana kwa Waislam, Al-Kaaba ni Qibla ya Waislam, Al-Kaaba kwa itikadi ya Kiislam ni nyumba ya Allah, Al-Kaaba kwa Itikadi ya Kiislam ndio nyumba ya kwanza iliyojengwa kwa ajili ya kumuabudu Allah; ni mahala patakatifu mno,” alisema.
Alisema aliyechora picha hiyo amefanya utovu wa nidhamu na kwamba ni hatari kwani si jambo jema kushambulia kitu kitakatifu kwa dini nyingine.
Alisema jambo linalofanana na hilo linaweza yanaweza kuamsha hisia za watu ambao utakuwa hatari kwa watanzania na kwa taifa, ambapo tayari kiongozi huyo akitambua yakwamba kuna sheria za mitandao.
“Tunatoa wito kwa TCRA kwamba kulinyamazia tukio hili ni kusababisha kuvunja utulivu na amani tuliyokuwa nayo katika ardhi ya Tanzania, sote tunatambua ya kwamba hakuna mivutano hatari na vita hatari na migongano hatari kama migongano ya wanadini,”alisema.
0 comments:
Post a Comment