Videos

Sakaya ahoji hatima ya wabadhirifu


Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya
MBUNGE wa Kaliua, Magdalena Sakaya CUF(pichani) ametaka kujua sababu ya Serikali kutoweka wazi hatua zilizochukuliwa kisheria dhidi ya waliohusika na ubadhirifu wa vyama vya ushirika katika mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na benki.

Akiuliza swali bungeni jana, Mbunge huyo alisema, Serikali ilifanya ukaguzi kwenye vyama vya ushirika mkoani humo pamoja na Chama Kikuu cha Ushirika (WETCU) tangu mwaka juzi na kubaini ubadhirifu mkubwa wa viongozi hao na benki mbalimbali.

“Kwa nini mpaka leo ripoti hiyo haijawekwa wazi, pia vyama vingi viko kwenye hali mbaya na havikopesheki na hivyo kusababisha wakulima kukosa pembejeo za kilimo, Serikali ina mpango gani mahususi wa kusaidia vyama vya ushirika kwa kuzingatia mchango wa tumbaku kwenye uchumi wa Taifa hili?” Alihoji Sakaya.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William ole Nasha alisema ripoti ya ukaguzi ilishakabidhiwa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kupitia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora tangu Septemba 18, mwaka juzi kwa Lengo la kuchukua hatua za kisheria dhidi ya makosa ya jinai yaliyobainika.

“Hadi Juni, maombi ya kuwafungulia mashitaka watuhumiwa yalishapelekwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DPP) akiridhia wafunguliwe mashitaka itafanyika hivyo,” alisema Nasha.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment