Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu |
Edith Msuya
OKTOBA 25, 2015 Watanzania walipiga kura na Rais John Magufuli akashinda kwa kura 8,082,935 (asilimia 58.46), akifuatiwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
OKTOBA 25, 2015 Watanzania walipiga kura na Rais John Magufuli akashinda kwa kura 8,082,935 (asilimia 58.46), akifuatiwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
Rais Magufuli atadumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitano, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mwingine mwaka 2020.
Ni utaratibu wa kisheria unaotoa fursa ya kufanyika Uchaguzi Mkuu kila baada ya miaka mitano, ukishirikisha vyama vingi vilivyorejeshwa nchini mwaka 1992. Ushindi wa Rais Magufuli umeendeleza mfululizo wa ushindi kwa wagombea wa nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Rais wa kwanza kushinda kupitia CCM baada ya kuingia kwa vyama vingi ni Benjamin Mkapa (awamu ya tatu), Jakaya Kikwete (awamu ya nne) na sasa Rais Magufuli. Uchaguzi Mkuu wa 2015 ulifanyika ikiwa ni miaka 23 tangua kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, hivyo kuwapo tofauti za kimazingira, uelewa na ushiriki wa raia katika mchakato wa uchaguzi.
Baada ya uchaguzi kupita, Serikali iliyopo madarakani ina haki za msingi kutekeleza ahadi zilizotolewa kwenye ilani ya uchaguzi ya chama tawala.
Lakini kwa vyama vingine vinapaswa kukutana, kupanga na kutekeleza mikakati ya kisiasa itakayowafikisha kwenye uchaguzi unaofuata, vikijiwekea mazingira bora ya kushinda. Ushindani wa aina hiyo kisiasa ni wenye tija kwa taifa lolote lililopo katika kipindi cha mpito katika nyanja tofauti ama zilizoendelea kiuchumi.
Kwa maana ni wakati ambapo watawala wanajiwajibisha kutekeleza ahadi zao ili waendelee kubaki madarakani, lakini wapinzani nao wakiangalia kwa ‘jicho la tatu’ ili kubaini udhaifu wa watawala, wautumie kwa kuomba ridhaa ya umma ili wachaguliwe.
Hivyo kila upande una haki za msingi kushiriki ujenzi wa taifa kupitia siasa. Watawala wanapaswa kutotumia vibaya mamlaka yao kuukandamiza upinzani, lakini na upinzani ukitakiwa kutumia mbinu na kauli za staha katika kuwakosoa watawala.
Ukandamizaji wa haki za raia kwa upande mmoja na matumizi ya lugha za kuudhi kwa upande mwingine, ni miongoni mwa vichocheo vya mafarakano, chuki na kuhatarisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Hapa nchini, hivi sasa kumekuwapo msuguano kati ya watawala na wapinzani. Wapinzani hususani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimefikia hatua ya kumuona Rais Magufuli kuwa kiongozi anayeongoza nchi kidikteta.
Ndio maana katika harakati za kisiasa, wakaanzisha vuguvugu la maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima kwa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania maarufu kwa kifupisho cha Ukuta.
Ingawa wapinzani wanaamini kudhibitiwa katika hatua za awali za ushiriki katika siasa baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015, lakini hiyo haiwezi kuwa kigezo cha kumkosoa mtawala aliyepo kwa kutumia lugha yenye kuudhi.
Ingawa kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili, baadhi ya maneo yana maana sanifu, lakini matumizi yake kwa kadri ya mazoea na mapokeo, yanafifisha hadhi ya mtu na wakati mwingine kudhalilisha utu wake.
Ndivyo ilivyo hata kwa mtawala anayetumia kiwango cha juu cha mamlaka yake kuwadhibiti raia wa kawaida wakiwamo wapinzani, ili wasipendekeze, wasiikosoe ama kuishauri serikali yake, haiwezekani kwa taifa la namna hiyo kupiga hatua za maendeleo.
Kwa maana hiyo, si kweli mtawala kama Rais Magufuli anaweza kusifika kwa mambo yasiyowapendeza watu hata wakafikia hatua ya kumuiuta dikteta.
Ni kweli kwamba Rais Magufuli hana mazuri yanayopaswa kutangazwa isipokuwa kumuona katika taswira ya kiongozi katili na mkali? Rais Magufuli amefanya mambo mengi ya msingi na yenye uthubutu ambao haujawahi kufanywa na viongozi wa miongo takribani minne, ukiondoa waasisi wa uhuru kwa mataifa ya Afrika akiwamo hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Lakini pia si kweli kwamba wapinzani ni wakorofi, watu waliobobea katika vurugu na kuhatarisha amani ya nchi.
Wapinzani wamechangia na bado wanachangia kwa kiasi kikubwa uboreshaji wa sera, sheria na mifumo tofauti ya kijamii ikiwamo ya uongozi wa umma. Wapinzani wameshiriki kikamilifu kuhoji kwa takwimu na uhalisia, na mara kadhaa wakiungwa mkono na wabunge ama kada nyingine ndani ya CCM ama serikalini.
Kuwaona wapinzani kwa mtazamo wa watu wenye vurugu, fujo na wasioitakia nchi mema, ni dhana potofu inayoweza kuifanya nchi kurudi nyuma kimaendeleo kutokana na kutoshiriki kwao kupitia shughuli za siasa.
Kwa hali hiyo, kila upande unapaswa kuweka mbele maslahi ya umma, ukijiwajibisha kwa uvumilivu katika kukosoana pasipo kugombana. Hiyo ndio Tanzania tangu wakati wa utawala wa hayati Mwalimu Nyerere.
Hivyo ni vizuri kwa wakosoaji wa Rais Magufuli wakaangalia namna bora ya kumkosoa kiongozi wa nchi ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa. Mathalani, kuna watu wanaopatikana kwenye mitandao ya kijamii wakitumia lugha ya kuudhi dhidi ya Rais wa nchi. Hali hii haipendezi.
0 comments:
Post a Comment