RAIS John Magufuli amemwapisha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), baada ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa jana kwa vyombo vya habari kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, uapishaji huo ulifanyika jana.
Taarifa hiyo ilisema Balozi Dk Dau (pichani) anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Balozi Dk Aziz Mlima ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kikanda.
Wakati huo huo, Rais Magufuli aliwaapisha makatibu tawala wa mikoa mitatu aliowateua mwishoni mwa wiki iliyopita.
Walioapishwa ni Eliya Ntandu anayekuwa Katibu Tawala wa wa Mkoa wa Songwe ulioanzishwa rasmi Februari, Adoh Mapunda anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.
Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Benedict ole Kuyan ambaye amestaafu, Tixon Nzunda anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Symthies Pangisa ambaye amestaafu.
Baada ya kuapishwa, Balozi Dau na makatibu tawala hao watatu walikula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili, Jaji mstaafu Salome Kaganda na kushuhudiwa na Rais Magufuli.
0 comments:
Post a Comment