Videos

Mbowe atupiwa samani nje na NHC kwa madeni



Leonce Zimbandu

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) linatarajia kupiga mnada mali za Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iwapo atashindwa kulipa deni la sh. Bilioni 1.172 kwa muda wa siku 14.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya  NHC kufuata taratibu zote za kisheria kwa  kutoa notisi ya siku 30  na kumalizika Agosti 29, mwaka huu na lakini mdaiwa alishindwa kulipa deni hilo.

Jana majira ya saa 07:00 NHC  wakiwa na  Kampuni ya udalali ya Fosters Action Mart walifika katika Ofisi za gazeti la Tanzania Daima na Club ya usiku ya  Bilicans na kutoa dhamani za ofisi nje ya jengo hilo.

Meneja wa Ukusanyaji kodi wa NHC, Japhet Mwanasenga aliyasema hayo  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa nje thamani  hizo jijini Dar es Salaam jana.

Alisema  mpango huo  kuwaondoa kwenye nyumba wadai sugu siyo  kwa Mbowe pekee bali wengine wanapaswa kujiandaa  kwa kulipa mapema  kodi  hiyo kabla ya rungu la sheria halijawafikia.

“Tumeanza kumdai kodi ya pango  Mbowe  tangu mwaka 1995  na kupewa muda wa kulipa lakini ameshindwa kulipa,   hivyo kilichobaki ni utekelezaji na suala hili halina siasa hata taasisi za serikali zinazodaiwa hatua zitachukuliwa, ikiwamo kuwaondoa,” alisema.

Alisema  Mbowe ni mpangaji kama wapangaji wengine wala hana  ubia na shirika hilo, kama ingekuwa hivyo angeendeleza kwa  kujenga Mbowe Hoteli  kama alivyojitambulisha kwenye Mkataba.

Mwanasenga aliendelea kusema kuwa hilo siyo suala la kisiasa  bali ni suala la kiutendaji kwa ajili ya kukusanya madeni yote iwe kwenye taasisi za serikali au binafsi.

Mkurugenzi wa  Kampuni ya Udalali ya Fosters Actionn Marts, Joshua Mwaituka alisema  kwa mujibu wa sheria yam waka 2005 inatoa fursa kwa NHC kumwondoa Mpangaji wake ikiwa atashindwa kutimiza masharti ya mkataba.

Alisema  wakiwa madalali wanaendeleza kufuata maelekezo ya mteja wao, hivyo watasubiri siku 14 zimalizike ili waanze kuuza mali hizo.

“Thamani zote za Mbowe zilizopo katika jengo la Mbowe Hoteli zipo chini ya Kampuni yangu kwa kuuzwa ikiwa mdaiwa atashindwa kuvikomboa ndani ya siku alizopewa,” alisema.

Agosti 24, mwaka huu Mbowe alisema amepata taarifa ya mkutano wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Waandishi wa habari kuhusu kilichoitwa “wadaiwa sugu” wa NHC ambapo katika orodha hiyo kampuni ambayo ina hisa ya Mbowe Hotels Co.Ltd imeorodheshwa kama mdaiwa anayedaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni moja.

Alikiri kuwapo kwa mgogoro wa kibiashara wa miaka mingi baina ya Kampuni hii na NHC lakini alisema kampuni hiyo imekuwa ikilipa kodi stahiki kwa NHC kwa mujibu wa makubaliano yao ya kibiashara.

Mbowe alidai kumekuwepo na ukakasi wa muda mrefu kuhusiana na mkataba  wa umiliki, uendelezaji na uendeshaji wa jengo hili unaochagizwa na msimamo wake wa kisiasa.

Haki na Uhuru  wa kufanya biashara kama raia wengine umekuwa ukiingiliwa mara kwa mara katika mazingira yanayoambatana na vitisho kiasi ambacho maamuzi kadhaa hayafanyiki kwa hofu ya kisiasa

Hivyo, alipenda umma wa Watanzania uelewe kuwa hadaiwi NHC.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment