MTENDAJI Mkuu wa Kampuni ya Quality Group, Arif Sheikh ametunukiwa Tuzo ya Kiongozi Mkuu-Fahari ya Taifa la India Mwaka 2016.
Sheikh ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Kampuni hiyo kubwa nchini Tanzania, ametukiwa tuzo hiyo juzi (Septemba 3) mjini Mumbai, India.
Amepata tuzo hiyo iliyotolewa na taasisi ya The Asia One Global Indian Leader, baada ya kuonyesha uwezo wa hali ya juu katika kubadili taswira ya sekta ya biashara nchini Tanzania.
Mbali na Sheikh, wengine waliopata tuzo hiyo ni Mwanzishili wa kampuni ya Dangote - Aliko Dangote, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Pepsi, Indira Nooyi na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Microsoft, Satya Nadela.
Pia, taasisi hiyo ikawatambua na kuwapa tuzo hiyo, Nita Ambani, Mshindi wa tuzo ya Nobeli, Prof Amartya Sen, Gautam Singhania na Raymond Group.
Kwa nini Sheikh?
Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh aliwashukuru wafanyakazi wenzake wa kampuni ya Quality Group Limited, hususan mtangulizi wake katika nafasi ya Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Yusuf Manji.
“Imekuwa ni heshima kubwa sana kwangu kupata tuzo hii ya kimataifa. Ingawa mimi ndiye niliyepewa tuzo hiyo, ninaitoa kuwa ni fahari ya kampuni ninayoiongoza ya Quality Group Limited. Nimefurahi kwamba nimeingia katika orodha ya watu waliowahi kupata tuzo hiyo ambao nimekuwa nikivutiwa nao sana.”
Sheikh alisema ametembea na kufanya kazi katika mabara mbalimbali, lakini kote hajaona kiongozi anayemvutia kama Rais John Magufuli ambaye ameapa kumuunga mkono katika jitihada zake mbalimbali za kuliletea maendeleo taifa la Tanzania.
Mashuhuda wasema
Mmoja wa watu waliohudhuria hafla hiyo alitaja kilichomfanya Sheikh afanikiwe kupata tuzo hiyo kuwa ni uwezo wake wa kuelimisha wengine kutumia taaluma zao kwa ajili ya kujiletea maendeleo endelevu.
“Amekuwa akifanya shughuli zake kwa kuwashirikisha wafanyakazi wenzake na ukiwauliza wafanyakazi wake watakwambia kuwa kufanya kazi na Sheikh ni ngumu lakini inakusaidia kujifunza,” alisema.
Kwa sasa Sheikh anakuza kipawa chake cha kuendesha biashara nchini Tanzania kwa kutekeleza miradi kadhaa ukiwamo mradi wa FastaFasta unaotoa huduma ya usafiri kwa kutumia pikipiki 60,000 na mradi wa kuendeleza Mji Mkongwe ambao utakapoingia katika hatua ya tatu, utakuwa moja ya miradi michache inayotoa ajira kwa Watanzania wengi.
Miradi mingine ni Pamoja worlds ambao ni mradi wa kwanza nchini Tanzania unaotoa huduma ya mtandao kwa Lugha ya Kiswahili, biashara mtandao na miradi mingine kadhaa katika sekta zinazoendelea kukua nchini humo ikiwamo sekta ya Elimu, afya, Teknolojia, mauzo ya nje, Magazeti, Kilimo Biashara na uchimbaji wa madini ambazo kwa pamoja zimeleta faida ya Dola Bilioni moja za Marekani
“Kwa pamoja miradi hiyo imeifanya Tanzania kuwa ni nchi yenye fursa nzuri ya kukua kiuchumi, kukuza ajira pamoja na kuwa eneo salama la uwekezaji wa kimataifa.”
0 comments:
Post a Comment