PADRE wa Kanisa Katoliki, Baptiste Mapunda, amesema viongozi wa dini kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Umoja wa Makanisa ya Kipentekosto na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) watakapokutana na Rais John Magufuli kujadili mustakhabari wa Tanzania, wawe wakweli na watumie busara badala ya kumungĆunya maneno ili kuiponya Tanzania.
Padre Mapunda wa Shirika la Mapadri la White Fathers, aliyasema hayo jana alipohubiri katika Ibada ya Misa Takatifu katika Parokia ya Manzese Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam na kusisitiza kuwa, bila viongozi wa dini kujitokeza huku wakiongozwa na hekima ya Mungu, ipo hatari taifa likaangamia kwa kuwa zipo dalili nyingi kwamba, mambo sasa hayaendi vizuri.
“Viongozi wa dini wakikaa kando na kusubiri mambo yaharibike watoe matamko, watakuwa hawalitendei haki taifa na mambo yakiharibika, hawawezi kukwepa lawama,” alisema.
Alikemea alichokiita tabia ya upotoshaji inayolenga kuwafunga midomo viongozi wa dini ili wasiseme ukweli hasa kukosoa kwa madai kuwa, kufanya hivyoni kuchanganya dini na siasa.
“Viongozi wa dini lazima wasome alama za nyakati; TEC, Bakwata na Wapentekoste, wachukue hatua kumshauri rais kwa busara na ujasiri ili kuliponya na kulinusuru taifa Wamshauri vizuri rais ili nchi iwe ya haki, upendo ma amani ya kweli. Wakienda kwa rais wamwambie ukweli si kumungĆunya maneno kwa kuwa, wao wakiwa manabaii, wanaona kwa jicho la Mungu,” alisema .
0 comments:
Post a Comment