Ofisa Uhusiano Mkuu wa Wakala wa Barabara za Serikali (Tanroads), Aisha Malima (kushoto), akijibu baadhi ya hoja katika mahojiano maalumu aliyofanya na jopo la waandishi wa habari na maofisa wa gazeti la Jambo Leo jijini Dar es Salaam leo.
Kutoka kulia kwa Aisha ni mwandishi wa habari mwandamizi, Moi Dodo; Mhariri wa Jambo Leo Wikiend, Joseph Lugendo; Meneja wa Masoko na Oparesheni wa Quality Media Group Limited, Peter Minja na Ofisa Mauzo wa kampuni hiyo, Desdery Christopher. Malima ametembelea ofisi za Jambo Leo zilizopo jengo la kibiashara la Quality Centre Barabara ya Nyerere, kwa lengo la kujenga ushirikiano. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
0 comments:
Post a Comment